for-the-first-time-ever-astronomers-detected-planets-outside-our-galaxy-in-2018

Umuhimu wa asali iliyo changanywa na mdalasin

Asali ni tiba karibu kwa kila ugonjwa. Matumizi ya asali kama tiba kwa magonjwa mbalimbali ni kitu ambacho kinafahamika kwa karne nyingi zilizopita duniani kote. Vitabu vingi vya zamani vimeandika namna watu walivyotibiwa magonjwa mbalimbali kutokana na asali.

Inapotokea dawa za asili mbili zinachanganywa pamoja katika uwiano fulani, hutokea kuundwa dawa nyingine nzuri ambayo ni tiba kwa maradhi mengi sana. Moja kati ya muunganiko wa dawa hizo za kushangaza ni pale asali inapochanganywa na mdalasini.

Muunganiko huu umekuwa ukitumika kwa karne nyingi kutibu magonjwa mengi mwilini na kuimarisha afya ya mwili kwa ujumla. Watu wengi wanakiri maajabu yaliyomo kwenye hii dawa asili ASALI YENYE MDALASINI.

Dawa hii ya asili ni maarufu kwa maelfu ya miaka katika tiba asili za China (Traditional Chinese Medicine – TCM), Ugiriki (Unani Medicine), India (ayurvedic) na Mashariki ya kati (The science of medicines based on natural treatment in the East – Tibb).

Kwa mjibu wa wataalamu wa tiba asili nchini China, mdalasini huongeza joto mwilini. Mdalasini hutengeneza joto mwilini lijulikanalo kwa kichina kama “yang”. Yang hutibu “yin” (yin kwa kichina humaanisha baridi). Wakati asali yenyewe kwa asili huweka sawa usawa wa joto na baridi mwilini.

Haya ndiyo maajabu 24 ya asali yenye mdalasini ulikuwa huyajuwi bado

1. HUUA BAKTERIA

Asali ina sifa ya kudhibiti bakteria. Nadharia hii inathibitishwa na tafiti nyingi kadhaa. Asali hupigana dhidi ya maambukizi ya ndani na ya nje. Mdalasini pia una sifa ya kuondoa vivimbe, pia huondoa sumu mwilini. Vinapoungana vitu hivi viwili vya asili vinatengeneza muungano mmoja mhimu wa dawa dhidi ya maambukizi ya nje.

2. NZURI KWA UGONJWA WA MOYO

Chakula sahihi, mazoezi ya viungo, na kuepuka kukaa kwenye kiti masaa mengi ni mhimu kwa ajili ya kuwa na afya nzuri ya moyo.

Kunywa kinywaji chenye asali yenye mdalasini mara kwa mara kunaweza kusaidia kuepuka ugonjwa wa moyo kwa kuzuia kuzibika kwa ateri.

3. INATIBU MAAMBUKIZI KWENYE KIBOFU CHA MKOJO

Asali yenye mdalasini ni dawa bora sana kwa kutibu maambukizi kwenye kibofu cha mkojo na bakteria wowote wanaoweza kushambulia kibofu cha mkojo.

Mchanganyiko huu unasafisha kibofu na kukiacha safi hivyo kukupa mazingira ya kutokuumwa lolote katika kibofu chako cha mkojo.

4. TIBA YA BARIDI YABISI (Arthritis)

Watu wengi wanaripoti matokeo mazuri baada ya siku chache tu za kutumia kinywaji hiki chenye mchanganyiko wa asali yenye mdasini kutwa mara 2.

Ili kutibu baridi yabisi ongeza kijiko kidogo kimoja cha mdalasini ya unga na kijiko kikubwa kimoja cha asali mbichi ndani ya glasi 1 ya maji ya uvuguvugu na unywe nusu glasi kabla ya chakula cha asubuhi na nusu glasi nyingine kabla ya kwenda kulala.

Utafiti huo ulifanyika katika chuo kikuu cha Copenhagen ambako wanafunzi walipewa asali yenye mdalasini ili kutibu baridi yabisi. Baada ya wiki 1 iligundulika kuwa wanafunzi 73 kati ya 200 walikuwa hawaonyeshi dalili tena za ugonjwa huo. Baada ya mwezi mmoja kila mmoja alikuwa amepona na kuwa na uwezo wa kutembea na kufanya kazi.

5. HUTIBU FIZI KUTOA DAMU

Watafiti nchini New Zealand wamegundua kuwa asali mbichi ikichanganywa na mdalasini inaleta ufanisi mkubwa dhidi ya fizi kutokwa damu, kuuma fizi, ganzi kwenye meno na maambukizi mengine katika fizi.

Unaweza kupakaa kwenye mswaki na utumie kama dawa yako ya kusafisha meno ili kupata faida hii.

6. INATIBU MENO YANAYOTOBOKA

Hii kidogo inashangaza. Watafiti katika jiji la New York nchini Marekani wanasema asali inaweza kusababisha meno kutoboka. Hata hivyo wanasayansi wengine nchini New Zealand wanasema asali inaweza kuwa msaada katika kuzuia meno kutoboka kutokana na sifa yake ya kuua bakteria mbalimbali.

Namna rahisi ni kutumia mchanganyiko wa asali yenye mdalasini kama dawa yako ya meno utumie kusafisha meno yako ili kuepuka meno kutoboka na kuoza pia.

7. HUSAIDIA MFUMO WA MMENG’ENYO WA CHAKULA

Husafisha utumbo mpana kwa kuondoa sumu na taka nyingine. Husaidia uzalishwaji wa bakteria wazuri kwenye utumbo mpana na kama matokeo yake huusadia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

8. HUONDOA GESI TUMBONI

Asali yenye mdalasini husaidia kulinda tumbo kwa kufunika kuta za tumbo. Kwa kusafisha mfumo wa bakteria wabaya huwa imesaidia kutibu maambukizi yoyote na hivyo kusaidia kutibu tatizo la tumbo kujaa gesi na asidi.

9. HUSAIDIA KUPUNGUZA UZITO

Kuna shuhuda nyingi zisizotiliwa shaka juu ya ufanisi wa asali yenye mdalasini katika kupunguza uzito. Asali na mdalasini vinapotumika pamoja, mchanganyiko huo huchoma mafuta kwa haraka sana.

Wakati huo huo mchanganyiko huu hushusha njaa na hivyo kumfanya mtu kujisikia ameshiba muda mrefu.

Angalizo hata hivyo, asali ni tamu na ina nguvu (kalori), hivyo ili kupunguza uzito unashauriwa usitumie zaidi ya vijiko vikubwa vitatu vya mchanganyiko huu ndani ya glasi moja ya maji ya uvuguvugu kwa siku, Ukizidisha tu unaweza kuongezeka uzito tena.

10. HUONGEZA AKILI

Watu wengi wanaripoti kuwa asali yenye mdalasini inawaongezea uwezo wao wa kukumbuka vitu. Asali yenye mdalasini hongeza uwezo wa ubungo kufanya kazi na kuongeza uwezo wa kumbukumbu.

11. HUTIBU KANSA

Ingawa bado haijathibitishwa kisayansi ni jinsi gani asali yenye mdalasini inatibu kansa lakini uwezo wake wa kuondoa sumu na vimelea vingine vya magonjwa (free radicals) kunaifanya kuwa na sifa hiyo ya kutibu kansa.

Baadhi ya watu wameripoti kupona kansa ya titi na kansa ya utumbo mpana kwa kutumia asali yenye mdalasini.

12. INAONGEZA NGUVU YA MWILI

Asali ina madini na vitamini nyingi ndani yake, wakati mdalasini wenyewe una kalsiamu, chuma, vitamini C, vitamini K, manganizi na nyuzinyuzi (fiber).

Vinapoungana vitu hivi viwili hufanya dawa moja mhimu sana ya kuongeza kinga ya mwili. Kunywa chai yenye asali na mdalasini mara kwa mara kunaongeza kinga ya mwili, nguvu ya mwili na nguvu ya ubongo kwa pamoja.

13. HUTIBU CHUNUSI

Kupakaa asali yenye mdalasini kwenye ngozi yako yenye chunusi kutaondoa chunusi hizo bila kuchelewa. Asali hudhibiti bakteria na mdalasini hudhibiti maambukizi kwenye ngozi na huondoa sumu.

Mchanganganyiko huu husaidia asali kubaki juu ya ngozi kwa muda mrefu na hivyo kufanya uponyaji unaohitajika.

14. HUTIBU KIKOHOZI

Kuinywa asali yenye mdalasini ndani ya glasi ya maji ya uvuguvugu hupunguza vyote kikohozi na kikohozi kikavu. Husafisha msongamano kohoni na kutibu kikohozi cha kawaida na hata kile kikavu.

15. HUZUIA MADHARA YA KUNG’ATWA NA WADUDU

Ni nzuri kwa ajili ya uvimbe au kuondoa maumivu yatokanayo na kuumwa na wadudu. Chukua kijiko kidogo kimoja cha asali na uchanganye ndani ya vijiko vidogo viwili vya maji ongeza na mdalasini ya unga nusu kijiko cha chai na upake juu ya sehemu ulipong’atwa na mdudu.

Maumivu hayo yataondoka mara moja.

16. HUSAIDIA KUOTESHA NYWELE

Changanya kijiko kidogo kimoja cha asali ndani ya ujazo sawa wa mafuta ya zeituni na uongeze kijiko kidogo cha chai tena cha mdalasini ya unga kwenye huo mchanganyiko.

Pakaa mchanganyiko huo kichwani sehemu ambako nywele zimeanza kupotea na uache kwa dakika 15 kisha jisafishe na maji ya uvuguvugu na shampoo ya asili.

17. HUTIBU LEHEMU (Cholesterol)

Matumizi ya mara kwa mara ya asali yenye mdalasini husaidia kupunguza lehemu. Pia husaidia kushusha shinikizo la juu la damu na kusafisha ateri zinazoziba.

Pia kubadili matumizi ya mafuta mengine na kuamua kutumia mafuta ya zeituni kutarahisisha kuweka sawa kolesto yako kirahisi zaidi.

18. HUTIBU MAUMIVU YA JINO

Changanya kijiko kidogo kimoja cha chai cha mdalasini ya unga na vijiko vikubwa viwili vya asali mbichi na upake kidogo kidogo juu ya jino linalouma mara kadhaa kwa siku kila siku mpaka maumivu yatakapopotea.

19. HUONDOA HARUFU MBAYA MDOMONI

Changanya kijiko kikubwa kimoja cha asali na kiasi kingine sawa cha mdalasini ya unga ndani ya maji glasi moja ya uvuguvugu na unywe mara tu ukiamka asubuhi.

Hii itakutibu tatizo la harufu mbaya mdomoni na utapumua vizuri bila shida yoyote.

20. HUTIBU UANITHI NA KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA

Jaribu na uone tofauti! Changanya vijiko vikubwa vitatu vya asali yenye mdalasini ndani ya glasi moja ya maji ya uvuguvugu na uache mchanganyiko huo kwa dakika 15 hivi.

Kunywa nusu glasi asubuhi kabla ya chakula cha asubuhi na nusu nyingine kabla ya kwenda kula kwa siku kadhaa hata wiki kadhaa.

21. HUONGEZA KINGA YA MWILI

Ongeza kinga yako ya mwili na magonjwa hayatakugusa. Vyote asali na mdalasini hupigana dhidi ya bakteria na virusi na hivyo kufanya dawa nzuri ya kupigana na kuua bakteria wabaya na virusi.

Asali pia ina madini na vitamini mhimu nyingi hivyo kuupa mwili viinilishe mhimu unaovihitaji.

22. HUTIBU MAFUA

Tumia mchanganyiko wa kijiko 1 cha chakula cha asali yenye mdalasini ndani ya glasi moja ya maji ya uvuguvgugu kutwa mara moja kila siku kuondoa chafya na kuvimba koo.

23. HUTIBU UGUMBA

Asali inaaminika kuamsha hamu ya mapenzi. Wapenzi wa jinsia zote wanashauriwa kunywa walau vijiko viwili vya chakula kila siku kabla ya kwenda kulala kila siku.

Mdalasini umetumika miaka mingi katika dawa za kichina na kihindi kuongeza uwezo wa uzazi kwa akina mama wenye kuhitaji kuzaa.

24. FAIDA NYINGINE LUKUKI

Kumbuka asali ni dawa karibu kwa kila ugonjwa na watu wamekuwa wakiitumia kutibu magonjwa mengine mengi bila idadi ikiwemo matatizo ya kisukari, kukakamaa kwa miguu na mikono, udhaifu wa jumla wa mwili, kuongeza kumbukumbu, vidonda vya tumbo, kutibu majeraha nk nk

Hayo ndiyo maajabu 24 ya asali yenye mdalasini ambayo ulikuwa huyajuwi bado.

Comments